UHERI WA DAUDI
“Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo, Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao. Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.” (Warumi 4:6-8)
Ni dhahiri kwamba Daudi hakujua zaidi kuhusu kipindi cha sasa cha “maongozi ya neema ya Mungu” kuliko Ibrahimu, na kwa hakika hakuwahi kuishi chini ya kipindi cha neema. Daudi aliishi chini ya kipindi cha Sheria, wakati ule dhabihu zilipohitajika ili kukubaliwa na Mungu. Kama Daudi angesema kwamba toleo la dhabihu halikuwa la lazima, bila shaka angepigwa mawe kulingana na Sheria.
Lakini Daudi, kinyume na wengi wetu leo, alielewa kusudi la Sheria ya Musa: kumleta mwanadamu katika hatia mbele za Mungu.
Katika Zaburi 130 alisema:
“BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ile Wewe uogopwe.”
Hakujua ni kwa jinsi gani Mungu angeweza kumwachilia kwa haki mwenye dhambi mwenye hatia, lakini aliamini kuwa ni jambo la kweli na alifurahia kwa Zaburi.
Katika Zaburi 32 alisema pia:
“Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.”
Mungu ni wa kushukuriwa, kwa kuwa sasa tunajua sababu!
Mungu amefunua kupitia kwa Mtume Paulo, mkuu wa wenye dhambi waliookolewa kwa neema, jinsi Yeye anavyoweza kuwa “mwenye haki, na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu” (Warumi 3:26).
Ni kwa sababu “Mungu alimfanya [Kristo] kuwa dhambi kwa ajili yetu, [Yeye] ambaye hakujua dhambi, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2 Wakorintho 5:21).
Uheri wa Daudi unaweza kuwa wetu pia, kama tutafanya kile ambacho Daudi alifanya:
Kumwamini Yeye ambaye kwa neema anasamehe dhambi na (kama tunavyojua sasa) huwahesabia haki waumini kwa msingi wa kazi ya ukombozi ya Kristo.
UTUKUFU NA UWEZA NA UKUU VINA YEYE HATA MILELE AMINA
Leave a Reply