HEKIMA YA ULIMWENGU HUU!
“Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?” (1 Wakorintho 1:20).
Changamoto hii ‘ilitupwa’ katika ulimwengu wa wenye ‘akili’ wa miaka 2000 iliyopita, maarufu sana kwa falsafa yake, fasihi na sanaa. Wala haya si maneno ya mtu ambaye yeye mwenyewe alikosa manufaa ya elimu ya juu. Badala yake, yalitiririka kutoka kwa kalamu ya mmoja wa watu walioelimika sana, mmoja wa wenye fikra kubwa wa wakati wote: Mtume Paulo. Zaidi ya hayo, yanapatikana katika Kitabu kile cha vitabu, Biblia, ambayo imestahimili, si kwa kadiri tu bali kwa utukufu, mashambulizi yote ya wakosoaji elfu elfu kwa karne nyingi za wakati. Kitabu hiki kinasema:
“Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu” (1 Wakorintho 3:19a)
“Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima” (Mithali 9:10)
Kwa hakika, “wasomi” katika zama zozote zile ni wale wanaokubali nadharia za wale wanaokubaliana wao kwa wao kuwa wao ni wasomi! Kama hukubaliani nao unakuwa umejipachika jina moja kwa moja kuwa hujui kusoma na kuandika; wewe sio ‘msomi’ kama wao!
“Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.” (1 Wakorintho 1:27-29)
UTUKUFU UNA YEYE MILELE NA MILELE AMINA
Leave a Reply