Home 2022 April 20 Unaweza Kuleta Tofauti Kubwa!

Unaweza Kuleta Tofauti Kubwa!

Unaweza Kuleta Tofauti Kubwa!

Mtu mmoja anaweza kuleta tofauti wakati wowote…

Katika ulimwengu wa kiroho, mara nyingi, mtu mmoja ameleta mabadiliko makubwa hasa mkono wa Bwana ukiwa juu yake:

  • Ni Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu, pekee ndiye aliyemficha mtoto Yoashi mwana wa Ahazia asiuawe, na kumwezesha kuwa mfalme mcha Mungu (2 Wafalme 11).
  • Eliya alisimama peke yake dhidi ya mamia ya manabii wa uongo, na mfalme mbaya na malkia (1 Wafalme 18).
  • Yonathani peke yake ndiye aliyemlinda Daudi kutokana na njama za mauaji za Sauli (1 Samweli 19).
  • Nathani alisimama peke yake ili kumkemea Daudi, akimshawishi kupata haki na Bwana (2 Samweli 12).

Mungu alimtumia mtu mmoja, Paulo, kukifichua kipindi chetu hiki kipya cha majira ya neema, na Onesiforo kumtia moyo Paulo wakati alipokabiliwa na majaribu makubwa (2 Timotheo 1:16-18):

“Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu; bali, alipokuwapo hapa Rumi, alinitafuta kwa bidii akanipata. Bwana na ampe kuona rehema machoni pa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonihudumia kwa mengi huko Efeso, wewe unajua sana.”

Mungu pia anaweza kukutumia wewe kuleta tofauti muhimu katika nyanja yako ya ushawishi, hasa katika kuishuhudia injili ya Neema ya Mungu; na hivyo kuleta mabadiliko kupitia huduma kwa wengine.

“Iweni hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake” (Waefeso 6:10)

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *