Home 2022 March 13 NEEMA Sio MALIPO!

NEEMA Sio MALIPO!

NEEMA Sio MALIPO!

Je, umewahi kugundua kwamba Mungu hawainui mbele yetu ‘watu wakuu’ (mababa) wa kwenye Maandiko kwa sababu ya wema wao binafsi?

Takribani mara zote, kumbukumbu zao zimeharibiwa na kushindwa kwao dhidi ya dhambi, lakini Mungu anatuamuru tuangalie imani yao, ili tuone na kujifunza kile ambacho imani yao iliwafanyia/iliwapatia. Hata wale ambao waliishi maisha mazuri (ya utii) mfululizo hawaletwi mbele yetu kwa sababu ya ‘thamani’ yao binafsi, kwa kuwa Mungu anajua kutokukamilika kwao. Hivyo Warumi 4:2-3 inasema hivi:

“Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa matendo, analo la kujisifu; lakini si mbele za Mungu. Kwa maana Maandiko Matakatifu yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.”

Na Mstari wa 6 unaendelea kusema juu ya Daudi:

“Kama vile Daudi aunenavyo uheri wa mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo.”

Hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kuishi maisha matakatifu kiasi cha kumfanya akubalike kwa Mungu, kwa kuwa, kwa Mungu ni ukamilifu pekee ndiyo unaotosha. Kama dhambi moja iliiharibu dunia na Mungu hakuinyamazia; Mungu pia hataruhusu dhambi moja iharibu mbingu…!

Hii ndiyo sababu, kwa neema, Mungu alimtoa Kristo aje afe kwa ajili ya dhambi zetu na kulipa malipo ya adhabu ya dhambi kwa haki, kwa ajili yetu. Ni kwa sababu ya malipo hayo ya kutosha haki yote yaliyofanywa na Kristo kwa niaba yetu, Mungu sasa anaweza kuwa “mwenye haki, na “mwenye kumhesabia haki” yule mwenye kuweka imani yake katika Kristo (Warumi 3:26).

Sura maarufu ya Waraka wa Paulo kwa Waebrania (Sura ya kumi na moja) inathibitisha ukweli kwamba wokovu, au kukubalika na Mungu; hupatikana, si kwa jitihada za kibinadamu, bali kwa imani. Sura hii kuu juu ya mashujaa katika “Jumba la Umashuhuri” la Mungu, inaanza kwa maneno haya:

“Maana kwa hiyo [imani] wazee wetu walishuhudiwa,” na kisha inaendelea: “Kwa imani Habili…,” “Kwa imani Henoko. …,” “Kwa imani Nuhu…,” “Kwa imani Ibrahimu…,” n.k., na inamalizia kwa tamko hili:

“… Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao…”

Utukufu na Wema na Uweza Vina Yeye Milele Yote; AMINA.

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *