Home 2021 May 02 Kwanini Mungu Anavumilia?

Kwanini Mungu Anavumilia?

Kwanini Mungu Anavumilia?

Mtakatifu Petro hakukosea alipotangaza katika siku ile ya Pentekoste kwamba siku za mwisho zimeanza (Matendo 2:16-17). Zilikuwa zimeanza kweli, lakini Mungu alikuwa na mpango wa SIRI wa kuupa ulimwengu kipindi cha NEEMA kabla ya ‘kuweka chini’ uasi wake na kumtuma Kristo kutawala.

Kusudi hili la siri kuhusu “wakati wa madaraka ya neema ya Mungu” ndio mada ya nyaraka za Mtume Paulo. Hatahivyo, inastaajabisha kuona jinsi ujumbe wa mwisho wa Mtume Petro unaelezea sababu ya ‘mkatizo’ huu katika mpango uliotabiriwa na Mungu na kucheleweshwa kwa kurudi kwa Kristo kutawala. Kwanza, anasema katika 2 Petro 3:8:

“Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja”

Angalia vizuri, haya sio maelezo yetu dhaifu ya sasa juu ya kuchelewa kurudi kwa Kristo. Kauli hii ilitolewa mwanzoni mwa wakati huu wa kungojea, alfajiri ya enzi ya neema!

Lakini hebu tuendelee na tamko la Petro:

“Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” (Mstari wa 9).

Kwa hivyo kucheleweshwa kwa kurudi kwa Kristo kuhukumu na kutawala haipaswi kuhesabiwa kama “uvivu” au ulegevu, bali uvumilivu. Kwa hivyo Mtume anaendelea kusema:

“Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu ni wokovu…”

Je! Petro alipata wapi habari hii? Alijuaje kuhusu “wakati wa madaraka ya neema ya Mungu”? Mstari wa 15 unaelezea:

“Kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa”

Kimsingi Mtume Paulo ndiye alipewa “injili ya neema ya Mungu” ambayo sisi tunaitangaza leo (Matendo 20:24). Mtume Petro alilitambua jambo hili (Wagalatia 2:2,7,9), na akafunga waraka wake ya pili kwa ushauri huu:

“Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo” (2 Petro 3:18)

Kwa utukufu wa JINA, lipitalo majina yote!

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *