Kumfuata Paulo
Kumfuata Paulo
Kwa nini unapaswa kufuata mfano ambao Bwana aliutoa kwetu kupitia kwa mtume Paulo? Sababu zipo nyingi, hizi ni baadhi:
Bwana Yesu Kristo ndiye aliyemtuma Paulo (Matendo 9:15).
Mungu aliamuru hivyo (1 Timotheo 1:1; 1 Timotheo 1:16).
Mungu alimfanya kuwa Mtume wako (Warumi 11:13).
Mungu alimpatia injili ya wasiotahiriwa (Wagalatia 2:7-9).
Kama umeokolewa, ni kwa injili yake ya Kristo (Warumi 16:25; 1 Wakorinto 15:1-4).
Petro alimpa Paulo haki za kipekee za huduma kwa wasiotahiriwa (Wagalatia 2:9).
Petro alimwinua Paulo katika masuala ambayo Bwana anafanya sasa (2 Petro 3:15).
Paulo anaagiza hivyo (1 Wakorinto 11:1; Wafilipi 3:17).
Kushindwa kufuata mfano wa Paulo …
… hupunguza mahubiri ya msalaba kwa ajili ya wokovu.
… nguvu ya msalaba hubadilishwa na kuwa nguvu ya matamanio.
… hupora utajiri wako wa kiroho katika Kristo Yesu.
… kunaendeleza ujinga wa mapenzi ya Mungu hivi leo.
… huudhohofisha Mwili wa Kristo kwa kuliweka Kanisa chini ya sheria na kulilinganisha na Israeli, katika kuwa na mahusiano yenye masharti na Mungu.
Si ajabu Paulo anatumia muda wake mwingi katika nyaraka zake kutangaza utume wake maalum.
“Basi, nawasihi mnifuate mimi” – 1 Wakorinto 4:16
Kwa Utukufu wa Jina la Yesu Kristo
Leave a Reply