Home 2020 February 05 Habari Njema

Habari Njema

Habari Njema

INJILI = Habari Njema!

Injili ni habari njema, lakini ni habari njema ipi inaifanya Injili kuwa habari njema?

Mengi ya yale yanayouzwa kama “injili” ni mbadala duni kwa jambo halisi. Usipumbazwe na punguzo la bei! Kuna njia rahisi ya kutofautisha jambo halisi kutoka kwa jambo lililo bandia. Injili ya kweli, ni 100% habari njema. Hakuna habari mbaya ndani ya habari njema. Kama injili ‘uliyoinunua’, ndani yake inakufanya ujisikie kuwa si-salama, una-wasiwasi, una-hatia, na una-kuhukumiwa, basi hiyo si habari njema. Itupilie mbali, kabla haijakuua!

Injili ya awali ilikuwa na furaha kubwa kwa watu wote. Ilikuwa, na bado, ni tangazo kuhusu MTU mmoja tu (ambaye si wewe wala mimi). MTU huyo hakufanyika tendo mmoja tu, bali matendo mawili yenye umuhimu mkuu na ni ya milele. Kama bado hujasikia kuhusu MTU huyo na MATENDO yake, basi hii itakuwa ni habari njema kwako:

Yesu alikufa kwa ajili yako

Katika kuonyesho upendo mkuu ambao ulimwengu hahujawai kuuona, Yesu alitoa maisha yake kwa ajili yetu, wakati tungali wenye dhambi (Warumi 5:8). Tulikuwa tumechagua kujitangazia uhuru kutoka kwa Mungu (hatukumhitaji Mungu), upepo wa kimbunga ukatupiga! Lakini Mungu alitupenda upeo kiasi kwamba alimtuma mwanawe ili aje kutulipia fidia kutokana na nguvu ya dhambi na kifo. Mwana wa Mungu akawa mwana wa Adamu na alichukua adhabu ambayo inatuletea amani kwa sababu ilitupatanisha na Mungu. Yeye alikataliwa ili sisi tuweze kukubalika; alijeruhiwa ili tuweze kuponywa; alilaaniwa ili sisi tupate kubarikiwa. Msalabani, yeye alizibeba dhambi zetu na akatupatia haki yake. Kupitia kwake, sisi tumekuwa na amani na Mungu, na dhambi zetu hazihesabiwi dhidi yetu. Katika ‘mtego’ wa kifo Yesu alilia, “imekwisha.” Mpango wake wa uokoaji (ukomboaji) ukakamilika, Yesu akaiweka Roho yake mikononi mwa Baba yake, akafa.

Yesu anaishi kwa ajili yako

Fidia ililipwa kwa ukamilifu, Yesu alifufuka katika ushindi kutoka kwa wafu. Sasa anaketi katika mkono wa kuume wa Baba, Kuhani Mkuu mkamilifu ambaye daima anaishi akizungumza kwa ajili yetu. Kama unaamini kwamba Yesu amekuokoa, basi mwamini kwamba yeye atakutunza na kamwe hatabadili mawazo yake. Yeye ni mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu (Waebrania 12:2) na damu yake imetupatia ukombozi wa milele. Yesu hayuko peke yake katika haya. Baba yako wa Mbinguni anakupenda kwa upendo usio na mwisho na kukuokoa ulikuwa ni mpango wake tangu milele yote. Ili tuweze kuwa na matumaini imara na salama, Mungu Baba ameapa agano la amani na Mwana wa Mtu na kamwe hawatalivunja (Waebrania 6:17-20). Yeye pia ametupa Roho wake Mkuu – Roho yule yule ambaye alimfufua Yesu kutoka kwa wafu – kama amana kuhakikisha yote aliyoyahidi. Kupitia kwa mwakilishi wetu Yesu, na kama udhihirisho wa upendo wake wa kudumu, Baba yetu wa Mbinguni amejiunganisha nasi, na ametuahidi kamwe hataondoka wala hatatuacha peke yetu. Sasa tunasimama salama, si juu ya ahadi zetu dhaifu kwake, bali juu ya ahadi zake zisizo na masharti na madhubuti kwetu.

Kwa UTUKUFU wa Jina lake…

Yesu 100% – Bila Nyongeza

Author: seta sanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *