Home 2020 February 03 Je ninini maana ya kumkubali Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa maisha yako?

Je ninini maana ya kumkubali Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa maisha yako?

Je ninini maana ya kumkubali Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa maisha yako?

Je, umeshawahi kumkubali Yesu kama mwokozi wako? Kabla hujajibu, niruhusu nikujibu kwanza swali moja,  kwa kuwa kwa kulielewa swali hili vizuri, ni vyema kwanza umwelewe vizuri Yesu Kristo, kibinafsi na kama Mwokozi. Swali ni kwamba, Yesu Kristo ni nani? Watu wengi humtambua Yesu Kristo kama mtu mzuri, Mwalimu Mkuu, au hata pia Nabii wa Mungu.

Haya maelezo yote huenda yakawa ni kweli kabisa kumhusu Yesu, lakini hayaelezei vizuri yeye ni nani. Bibilia inatuambia ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili, Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Tazama Yohana 1:1, 14). Mungu alikuja ulimwenguni kutufundisha, kutuponya, kuturekebisha, kutusamehe na kufa kwa ajili yetu! Yesu Kristo ni Mungu, Muumbaji, Mungu Mkuu.

Je umemkubali huyu Yesu? Je, Mkombozi ni nani na kwanini tunahitaji Mkombozi? Bibilia inatuambia ya kwamba sote tumefanya dhambi, sote tumetenda maovu (Warumi 3:10-18). Kutokana na dhambi zetu, basi tulistahili hasira za Mungu na pia hukumu. Adhabu ya pekee kwa kufanya dhambi ni adhabu isiyokuwa na mwisho au mipaka (Warumi 6:23; Ufunuo wa Yohana 20:11-15). Hii ndio sababu tunahitaji Mkombozi! Yesu Kristo, alikuja duniani na akafa badala yetu. Kifo chake Yesu, kama Mungu katika mwili, kilikuwa ni malipo yasiyokuwa na mwisho kwa ajili ya dhambi zetu (2 Wakorintho 5:21). Yesu alikufa ili kutulipia mshahara wa dhambi zetu (Warumi 5:8). Yesu alitulipia deni ili tukaweze kuwa na uhuru. Kufufuka kwake Yesu katika wafu kulidhihirisha ya kwamba kifo chake kilitosha kulipa mshahara wa dhambi zetu. Hii ndiyo sababu kwamba Yesu Kristo ndiye Mkombozi peke yake (Yohana14:6; Matendo 4:12)!

Je, unamwamini Yesu kama mwokozi wako? Je, Yesu ni Mwokozi wako? Wa Kibinafsi? Watu wengi huchukulia kwamba ukristo ni kuhudhuria kanisani, Kutoa sadaka, au kutofanya dhambi fulani. Huo siyo Ukristo! Ukristo wa kweli ni ule uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo. Kumkubali Yesu kibinafsi kama mwokozi wako inamaanisha kuweka imani yako kibinafsi kwake na kumwamini yeye. Hakuna aokokaye kupitia imani ya wengine. Hakuna asamehewaye kwa kutenda matendo aina fulani. Njia ya pekee ya wokovu ni kumkubali Yesu Kristo kibinafsi kama mwokozi wa maisha yako, kuamini kifo chake kama malipo ya dhambi zako, na kufufuka kwake kama hakikisho kwako la uzima wa milele (Yohana3:16).

Je, kibinafsi umemfanya Yesu Kristo kuwa Mwokozi wako? Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kibinafsi kama Mwokozi wako, hebu yaseme maneno haya kwa Imani kwa Mungu. Kumbuka, si kwa kuomba ombi hili au ombi lengine lolote lile ndiko kutakako kupa uokovu. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee yake ndiko kuwezako kukuokoa toka dhambini na kukupa uzima wa milele. Ombi hili ni kwa kumwelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupa huo wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume na mapenzi yako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyostahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa dhambi hizo. Natangaza kwamba naziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ninamkubali Yesu kibinafsi kama Mwokozi wangu! Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha huu mkuu, Amina”!

Author: magebo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *