Home 2020 February 03 Je Ninawezaje Kupokea Msamaha wa Dhambi Kutoka kwa Mungu?

Je Ninawezaje Kupokea Msamaha wa Dhambi Kutoka kwa Mungu?

Je Ninawezaje Kupokea Msamaha wa Dhambi Kutoka kwa Mungu?

Kujibu swali hilo, ni vyema tuanze kwa kusoma Kitabu cha Matendo 13:38-39 ambacho kinasema hivi, “Basi na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi; na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa”. Msamaha ni nini na kwanini ninauhitaji? Neno samehe linamaanisha kusafisha nia au jambo na kulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, kuachilia au kufutilia mbali kosa au deni.

Tunapomkosea mtu, tunaomba msamaha kwake ili turudishe uhusiano uliokuwepo kabla. Msamaha hautolewi kwa sababu mtu anastahili kusamehewa, la hasha, kwani hakuna mtu anayestahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia jambo ndani yako kinyume cha mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani. Bibilia inatuambia kwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20 inasema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi”. 1Yohana 1:8 inasema “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani mwetu”. Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4).

Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote vile msamaha wa Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika hukumu na adhabu ya milele tukiteseka kama matokeo ya dhambi zetu (Mathayo 25:46; Yohana 3:36). Namna ya kuupokea Msamaha unatakiwa upokelewe Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma kwetu, ni mwenye nia ya kutusamehe dhambi zetu zote! 2Petro 3:9 inasema, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba”. Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo ni jukumu letu kuupokea msamaha wetu kutoka kwake kwa moyo wa shukurani, ni neema yake tu ndiyo imetuokoa.

Adhabu na haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti”. Mauti ya milele ndiyo tuliyostahiri kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu – Yesu Kristo (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa msalabani kwa kuichukua adhabu ya kifo ambayo kwanza tulistahili sisi, yaani mauti. 2 Wakorintho 5:21 inatufundisha kuwa, “Yeye asiyejua dhambi alimfanywa kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye”. Yesu alikufa msalabani, akiichukua adhabu tuliyo stahili! Mungu, kwa kifo chake Yesu, alitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 inasema hivi, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote”. Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu ya dhambi na mauti (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, maana ndio ushindi wetu, Warumi 6:23 inasema “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Je, unatamani dhambi zako zisamehewe? Je, una hisia za kuzichukia dhambi zako mara kwa mara, na je unayo hukumu moyoni mwako, na je unatamani Mungu akusaidia tatizo lako hilo? Tumaini lipo, msamaha wa dhambi zako upo, lakini sharti tulilowekewa ni kumwamini tu Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yetu. Waefeso1:7 inasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake”. Yesu alitulipia deni lile tukapate kusamehewa na kuhesabiwa haki. Unacho takiwa kufanya ni kumwomba Mungu akusamehe dhambi zako kupitia kwake Yesu Kristo, ukiamini ya kwamba Yesu alikufa ili upate msamaha wa dhambi, naye atakusamehe! Yohana 3:16-17 ina habari hii njema sana, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye”.

Author: magebo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *