“Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anaishi kwa vinywa vyetu, twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu”
– 2 Wakorinto 5:20
Madhumuni Yetu
Lengo letu ni kuhimiza huduma ya uaminifu kwa Mungu kupitia mafundisho ya Yesu Kristo sawasawa na Ufunuo wa ile SIRI.
“Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injli yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele”
– Warumi 16:25
Tunamhubiri Yesu Kristo, upatanisho kupitia damu yake, haki tuliyohesabiwa kutokana na ufufuko wake, maisha yenye ushindi yaliyofanywa ndani yetu kwa imani.
Tunafundisha Biblia haina makosa, tukiigawa kweli ya Neno la Mungu, tukiheshimu maagizo ya Mtume Paulo ya kuigwa kweli hiyo ya Neno la Mungu sawasawa.
Tunawafikia kwa huruma, watu wenye dhambi na waliokufa katika dhambi tukiwa na matumaini kwamba nao watakombolewa kama sisi, kwa neema ya Mungu, ili wawe na uzima wa milele.
“ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli” – 1 Timotheo 2:4
Fundisho Letu
Mafundisho yetu na Mahubiri yetu yanaanza na kukamilika katika Kristo Yesu, Bwana na Mwokozi wetu. Ikiwa ni kutoka kitabu cha Mwanzo mpaka Sheria ya Musa, kutoka Injili ya Ufalme mpaka ufunuo wa ile Siri, tunamhubiri Yesu Kristo pekee kuwa ndiye YOTE katika YOTE. Tunatambua kwamba Kristo alimteua na kumtuma Paulo kuwa Mtume wetu katika majira haya ya sasa. Hivyo ni katika maandishi ya Paulo pekee ndimo tunamopata fundisho, hadhi, mtembeo na hatima ya Kanisa – Mwili wa Kristo.
Kwao wenye masikio ya kusikia, tunawafundisha kwa ujasiri, kuanzishwa kwa Kanisa (Mwili wa Kristo) baada ya kuitwa Mtume Paulo (mid-Acts Pauline dispensation) huko tukiligawa Neno la Mungu kwa usahihi!
Tunachoamini
Katika kuenenda katika Neema ya Mungu iliyoachiliwa, huku tukiwa ni mabalozi wa ushirika wa Mungu