“…wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi;… Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanya kwa ajili ya roho zenu…” – 2 Wakorinto 12:14-15
Tunafuata kielelezo cha neema kwa Paulo katika kupokea zawadi kwa huduma yetu. Paulo kamwe hakuomba pesa kwa ajili ya matumizi yake mwenyewe, ili kwamba Injili ya Kristo isije ikazuilika (1 Wakorinto 9:12). Wala sisi nasi, hatufanyi HIVYO!
Alitaka utoaji wa sadaka uwe ni tunda la neema itendayo kazi ndani ya mtoaji:
“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” – 2 Wakorinto 9:7
“Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu” – Wafilipi 4:17.
Ukurusa huu, umetengenezwa kutokana na maswali ya wengi wanaotaka kujua namna ya utoaji sahihi lakini pia kuacha kutoa kwa sababu ‘mbaya’.
Tunaomba uelewa kwamba, sisi hatuna ‘hamu’ ya fedha yako, bali wokovu wako na huduma kwa Bwana kwa moyo wa haki, tukizungumza ujumbe sahihi, kutoka kwenye Biblia sahihi, huku tukiigawa kweli ya Mungu sawasawa (Matendo 20:33-35).
Kama umeponzwa na mafundisho ya sheria ambayo yanakupa ahadi ya baraka kwa sababu ya kutoa zaka yako kwenye Kanisa lako, tafadhali tunakuomba uacha mara moja, kwani kwa kufanya hivyo, unaidharua kazi timilifu ya Msalaba wa Kristo!
Kama unakusudia katika moyo wako, kutoa kwa uhuru kwa huduma yetu ya neema kwa wengine, tafadhali endelea hivyo katika roho ya 2 Wakorinto 9:7. Asante kwa ukarimu na usaidizi wako.
Matumizi ya Sadaka na Michango
Sadaka, zawadi na michango mbalimbali inayotolewa hapa hutumiwa kulipia gharama za kueneza Injili ya Neema ya Kristo katika maeneo mbalimbali kama vile vipindi vya Radio, Magazeti, TV, Tovuti hii, kusaidia Wajane, Yatima na maeneo mengine mengi kwa Utukufu wa Jina la Kristo Yesu.
Akaunti Namba: 0150408542400
Jina la Akaunti: The Grace Walk Ministry
Jina la Benki: CRDB Bank PLC Ltd