Home 2024 September 25 MUNGU ALIYE HAI

MUNGU ALIYE HAI

MUNGU ALIYE HAI

“Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?” (Zaburi 42:2)

Nadharia ya hivi karibuni kwamba “Mungu hayuko hai” haijawa na faraja ya kweli wala uradhi kwa wale wote walio katika shida na/au huzuni.

Kwa miaka mingi sasa, imekuwa ikidhaniwa kwamba, maneno “Mungu aliye hai,” katika kifungu tajwa hapo juu, yalikuwa yanarejelea uwezo wa Mungu wa kusaidia, tofauti na sanamu mfu za kipagani zisizokuwa na nguvu za kuponya wala kuokoa. Uchunguzi wa makini wa muktadha husika wa andiko hilo, hata hivyo, unatuongoza kuamini kwamba, maneno hayo, yanahusika zaidi na uwezo Wake wa kujibu. Miungu ya kipagani, kinyume chake, ipo kama wanasesere wa watoto; haiwezi hata kujipepesa au kujibu kwa njia yoyote ile.

“Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu. Zina vinywa lakini hazisemi, zina macho lakini hazioni, zina masikio lakini hazisikii, wala hamna pumzi vinywani mwake” (Zaburi 135:15-17)

Lakini Mungu wa kweli, ni Mungu aliye hai; Ambaye anaona, anasikia na anajibu. Mtunga Zaburi, katika Zaburi 42, anajilinganisha na ayala, aioneavyo shauku mito ya maji kwa sababu ya kiu kali. Wakati mwingine, inadaiwa kuwa, eneo hilo linaonyesha mmoja wa ayala anayefukuzwa (anayewindwa), lakini kifungu hicho hakisemi chochote kuhusu hili. Israeli/Palestina ni nchi kavu, na bila hata kuwindwa, ayala anaweza kutamani sana vijito vya maji yanayotiririka…

Kimsingi, ayala, katika kifungu hiki, hatafuti msaada; bali ana kiu ya kuburudishwa, na ndivyo Mtunga Zaburi alivyotamani burudisho la ushirika na Mungu, Mungu aliye hai.

Je! Ni jambo jema kiasi gani, pale tunapoweza kumjua Mungu aliye hai, kwa kupitia imani katika Kristo Yesu? Hii ndiyo sababu, Mtume Paulo, katika Waebrania 10:19-20, anatangaza haya:

“Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake”

Kwa kifo chake, pale Kalvari, Bwana wetu Yesu Kristo alipasua lile pazia lililotuzuia kuingia katika uwepo wa Mungu, na sasa kwa kuitikia kiu yetu (shauku yetu), anasema:


честные казино с быстрыми выплатами
бездепозитные бонусы казино
играть в лучшем казино на деньги
база казино с бездепозитным бонусом
онлайн казино России
casino oyunu

“Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji” (Waebrania 4:16)

NAAM, MUNGU WETU NI MUNGU ALIYE HAI!

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *