Home 2024 August 14 BETHLEHEMU NA KALVARI!

BETHLEHEMU NA KALVARI!

BETHLEHEMU NA KALVARI!

“Jina tamu limeshuka kutoka Mbinguni juu,

Ili kuushinda upendo wa kina wa mioyo yetu;

Kama vile Bethlehemu na Kalvari inavyothibitisha: Yesu wangu.”

Wimbo huu wa zamani una ukweli mwingi! Bethlehemu na Kalvari zinathibitisha ukweli kwamba Bwana wetu Yesu Kristo alikuja kutoka mbinguni ili kutuvuta kwake.

Tamko la Mtakatifu Paulo kwamba “Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi” (1 Timotheo 1:15), linajumuhisha yote – Bethlehemu na Kalvari. Huko Bethlehemu Kristo alionyesha upendo wake kwa mwanadamu, si tu kwa kuja na kuwa pamoja nasi, bali pia ili awe mmoja wetu.

Luka, “tabibu mpendwa,” aliandika Injili maarufu – “Injili kama ilivyoandikwa na Mtakatifu Luka” – ili kuonyesha jinsi Bwana wetu Yesu Kristo alivyokuwa mwanadamu halisi. Mbali na dhambi, Bwana wetu alikuwa na hisia zote, huzuni, furaha, maumivu, raha, n.k., kama ambavyo tulivyo navyo sisi. Mwana wa Mungu, hakika alifanyika kuwa Mwana wa Adamu ili wanadamu wapate kuwa wana wa Mungu.

Lakini, maisha yake peke yake, hayangeweza kutuokoa; Utakatifu wake, ungefichua tu dhambi zetu na kutuhukumu! Hii ndiyo sababu Mtume Paulo anatangaza kwamba “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu” (1 Wakorintho 15:3), na kwamba katika yeye huyo, “TUNAO UKOMBOZI KWA DAMU YAKE, MASAMAHA YA DHAMBI, KWA KADIRI YA UTAJIRI WA NEEMA YAKE” (Waefeso 1:7).

Wale wote wanaoliamini hili na kumwamini Kristo Yesu kama Mwokozi wao binafsi wa maisha yao, wanafurahia ukweli wa utenzi uliopo hapo juu na kwamba mioyo yao imevutwa kwa yule Mbarikiwa aliyetoka mbinguni hadi Bethlehemu na Kalvari kwa sababu YEYE aliwapenda upeo.

Utukufu una Yeye KRISTO YESU Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *