Aya 104 Zinazokinzana katika Biblia
Mungu hajawahi kuweka makosa katika Biblia. Hata hivyo, kuwepo kwa miktadha na majira tofauti huunda mistari inayopingana katika Biblia. Ukinzani huu hufanya isiwezekane kamwe kutii kila agizo lililomo katika Biblia. Ni jambo la lazima kwa kila muumini kuyagawa kwa usahihi maagizo ya Bwana kwetu katika majira ya neema dhidi ya maagizo ya wakati uliopita au dhidi ya yale ya miaka ijayo.
Ni jambo lililozoeleka miongoni mwa waamini kutenganisha kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Lakini kinyume na hayo, Maagano yote mawili ni ‘mada’ juu ya unabii kwa Israeli. Habari ya siri aliyopewa Paulo inataka mgawanyo mwingine tofauti na ule uliotabiriwa.
Tunaweza kuzipatanisha tu, zile zinazosemwa kuwa ni tofauti, kwa kutambua ni nani anazungumza, kwa nani anazungumza, na chini ya muktadha gani wa majira anazungumza.
Ukinzani Juu ya Injili
- Je! Injili ni msalaba au ufalme?
- Marko 1:14-15 & 1 Wakorintho 15:1-4
- Je! Msalaba ulikuwa mtukufu au wa aibu?
- Matendo 3:13-15 & Wagalatia 6:14
- Je! Injili ilifahamika au ilikuwa siri?
- Warumi 16:25 & Matendo 3:21
- Je, wale kumi na wawili waliielewa injili au la?
- Luka 9:2 & Luka 18:34
- Je! Tunahubiri injili ya ufalme au ya Neema?
- Luka 9:2 & Matendo 20:24
- Je! Kuhesabiwa haki ni bure au ni kwa matendo?
- Warumi 4:5 & Yakobo 2:24
- Je! Damu ya Kristo ilimwagika kwa ajili ya wengi au wote?
- Mathayo 20:28 & 1 Timotheo 2:6
- Je! Dhabihu za wanyama huondoa dhambi?
- Walawi 16:27 & Waebrania 10:4
- Je! Mungu anatuhesabu dhambi dhidi yetu?
- Matendo 5:1-10 & Warumi 4:8
- Je! Tunahitaji matendo (kazi) kwa ajili ya kupata haki?
- Yakobo 2:24 & Tito 3:5
- Je! Wokovu haupatikani kwa matendo au kwa tabia zetu?
- Waefeso 2:8-9 & Luka 10:25-29
- Je! Ibrahimu alihesabiwa haki kwa matendo au si kwa matendo?
- Yakobo 2: 21-23 & Warumi 4:2-3
- Je! Dhambi zinasamehewaje?
- Yohana 20:23 & Wakolosai 1:14
- Je! Msamaha wa dhambi una masharti au hauna?
- Mathayo 6:14-15 & Waefeso 4:32
- Je! Neema ni nyingi zaidi au kuna dhambi isiyosameheka?
- Marko 3:29 & Warumi 5:20
- Je! Injili ni kuamini au ni kuwa na toba na ubatizo?
- Matendo 2:38 & Matendo 16:31
- Je! Tuna amani na Mungu?
- Mathayo 3:7 & Warumi 5:1
Ukinzani Katika Ubatizo
- Je! Tumetumwa kubatiza?
- 1 Wakorintho 1:17 & Marko 16:16
- Je! Injili inajumuisha ubatizo wa maji?
- 1 Wakorintho 15:1-4 & Marko 1:4
- Je! Ubatizo mmoja au ni zaidi ya mmoja?
- Waefeso 4:5 & Mat 3:11
Ukinzani Wa Wito
- Je! Nendeni kwa ‘watu wote’ au kwa Israeli tu?
- Mathayo 10:5-6 & Tito 2:11
- Je! Inapaswa kubeba pesa au la?
- Luka 10:4-5 & Luka 22:35-36
- Je! Wanafunzi walipaswa kwenda kwa mataifa yote au kwa watu wa tohara tu?
- Mathayo 28:19 & Wagalatia 2:9
- Je! Mtume Paulo alitumwa kubatiza?
- Mathayo 28:19 & 1 Wakorintho 1:17
- Je! Wamebatizwa na Yesu au katika Yesu?
- Yohana 4:1 & Warumi 6:3
- Je! Tunapaswa kushuhudia huduma ya Kristo hapa duniani?
- 2 Wakorintho 5:16 & Matendo 1:22
- Je! Petro alipaswa kuchukua upanga?
- Luka 22:36 & Mathayo 26:52
- Je! Tunapaswa kutafakari juu ya nini cha kusema?
- 1 Timotheo 4:15 & Luka 21:14
- Je! Roho Mtakatifu ndiye anayetamka au sisi?
- Matendo 6:9-10 & Wakolosai 4:6
- Je! Wapingaji wanaweza kupinga?
- Luka 21:15 & Tito 1:9
- Je! Ni Paulo au Petro ndiye mjenzi wa Kristo?
- Mathayo 16:18-19 & 1 Wakorintho 3:10
- Je! Paulo ndiye mdogo au ‘mkuu zaidi’ wa Mitume?
- 2 Wakorintho 11:5 & 1 Wakorintho 15:9
- Je! Paulo alikuwa wa kwanza au wa mwisho?
- 1 Wakorintho 15:8 & 1 Timotheo 1:16
- Je! Tunajuaje cha kusema na kuamini?
- Marko 13:11 & 2 Timotheo 3:15-17
Ukinzani Kuhusu Sheria
- Je! Tuko chini ya sheria au hatupo chini ya sheria?
- Mathayo 5:19 & Warumi 6:14
- Je, utunzaji wa Sabato unahitajika leo?
- Kutoka 20:8-10 & Wakolosai 2:16
- Je! Tohara ni ya muhimu?
- Mwanzo 17:10-14 & Wagalatia 5:2-6
- Je! Sheria inawahusu watu wenye haki?
- Mathayo 5:17-18 & 1 Timotheo 1:7-8
- Je! Tumeifia Torati au tunapaswa kuifuata?
- Mathayo 23:1-3 & Warumi 7:4
- Je! Haki huja kwa sheria?
- Kumbukumbu la Torati 6:25 & Warumi 10:3-5
- Je! Sheria ni ishara ya nguvu au udhaifu?
- Yoshua 1:7 & Wagalatia 4:9
- Je! Tunapaswa kutoa zaka?
- Mathayo 23:23 & 2 Wakorintho 9:7
- Je! Kutoa (zaka) ni hitaji linalostahili adhabu?
- Malaki 3:8-9 & 2 Wakorintho 9:7
- Je! Sheria za Sabato zinapaswa kushinikizwa?
- Hesabu 15:32-36 & Gal 4:10-11
- Je! Sheria inaleta uhuru au utumwa?
- Mathayo 23:1-2 & Wagalatia 5:1
- Je! Tunahitaji hekalu?
- Matendo 2:46 & 1 Wakorintho 3:16
- Je! Sheria za chukizo bado zinafaa?
- Mathayo 24:15 & Wagalatia 4:9-11
- Je! Tuna usalama katika Kristo au tunategemea tabia zetu?
- 2 Timotheo 2:13 & Waebrania 10:26-27
Ukinzani Kati ya Myahudi na Mmataifa
- Je! Kuna tofauti kati ya Myahudi na Mmataifa?
- Mathayo 15:26 & Wagalatia 3:28
- Je! Wayahudi waliokoa ‘kwa wakati ufaao’ au ‘nje ya wakati unaofaa’?
- 1 Pet 5:6 & 1 Wakorintho 15:8
- Je! Wokovu ni wa Wayahudi au wa Mataifa?
- Yohana 4:22 & Warumi 11:11
- Je! Baraka kwa Mataifa ni kwa kupitia kupanda au kuanguka kwa Israeli?
- Matendo 3:25 & Rum 11:11
- Je! Mataifa wataupokea wokovu?
- Matendo 28:28 & Warumi 1:28
- Je! Bwana aliwaambia mitume waende kwanza Yerusalemu?
- Luka 24:47 & Wagalatia 1:17
- Kristo yuko mkono wa kuume kwa ajili ya nani?
- Matendo 5:31-32 & Waefeso 1:19-23
- Je! Wasikilizaji wa injili ni akina nani?
- Mathayo 10: 5-7 & 2 Timotheo 1:11
- Je! Tumeokolewa katika taifa moja (Israeli) au Mwili mmoja?
- Isaya 60:3 & Waefeso 2:16
- Je! Sisi ni sehemu ya uzao au tumepokea hali ya kuwa wana?
- Mwanzo 9:9 & Wagalatia 4:5
- Je! Tunaifuata ipi? Huduma ya Yesu kwa Waisraeli au huduma ya Paulo kwa watu wa mataifa?
- Warumi 15:8 & 15:16
- Je! Paulo alikuwa na ‘imani ya pamoja’ na Warumi wasiotahiriwa au na huduma ya Yesu kwa watu wa tohara?
- Warumi 1:12 & Warumi 15:8
Ukinzani kati ya Unabii na wa Siri
- Je! Siri zilifunuliwa kabla ya kifo cha Kristo?
- Mathayo 13:11 & 1 Wakorintho 2:7-8
- Je! Ni nini kilichoandaliwa kabla/tangu ulimwengu kuwako?
- Mathayo 25:34 & Waefeso 1:3-4
- Je! Kazi ya Yesu ilitabiriwa au ilifichwa?
- Luka 24:44 & Waefeso 3:9
- Je! Ujumbe wa leo ulikuwa ukijulikana na manabii?
- Matendo 3:24 & Wakorintho 1:26
- Je! Tunaweza kuelewa vitu ambavyo Mungu ametuandalia?
- Isaya 64:4 & 1 Wakorintho 2:10
- Je! Kitabu cha Matendo ya Mitume kilikuwa ni mwisho au mwanzo?
- Matendo 2:17 & 1 Tim 1:16
Ukinzani Juu ya huduma yetu kwa Mungu
- Je! Ni nani anayewajibika na roho zetu?
- Waebrania 13:7 & Warumi 14:12
- Je! Tunampata Roho Mtakatifu wakati wa kuamini au ubatizo?
- Matendo 2:38 & Waefeso 1:13
- Je! Tunahitaji kukiri dhambi ili kupata msamaha?
- 1 Yohana 1:9 & Wakolosai 2:13
- Je! Tunaweza kula wanyama?
- Mwanzo 1:29-30 & Mwanzo 9:3-4
- Je! Tunaweza kula wanyama gani?
- Kumbukumbu 14:3 & 1 Timotheo 4:4
- Je! Tunapaswa kuuhifadhi umoja au kudumisha utengano?
- Waefeso 4:3 & Warumi 16:17
- Je! Tuwe kama chungu au kama kunguru?
- Methali 6:6-8 & Luka 12:22-24
- Je! Tunapaswa kufanya kazi kwa ajili ya chakula au la?
- Mathayo 6:25-26 & 1 Tim 5:18
- Je! Tunapaswa kuuza vyote au tutoe mahitaji kwa familia zetu?
- 1 Tim 3:5-6 & Marko 10:17-22
- Je! Tunapaswa kuhukumu?
- Mathayo 7:1-2 & 1 Wakorintho 2:15
- Je! Watumishi wa Mungu wanapaswa kufanya kazi kwa chakula?
- Luka 10:4-5 & 2 Wathesalonike 3:8-11
- Je, kuwa na mtoto ni jambo jema au baya?
- Mathayo 24:19 & 1 Timotheo 5:14
- Je! Roho Mtakatifu hubaki kwetu au huondoka tunapokosea?
- Zaburi 51:11 & Waefeso 4:30
- Je! Tunahitaji mwalimu?
- 1 Yohana 2:27 & 2 Timotheo 2:2 & Waefeso 4:11
Ukinzani Juu ya Matukio ya Baadaye
- Je! Amani duniani au la?
- Luka 2:14 & Luka 12:51
- Je! Wayahudi wana sehemu maalum mbele za Mungu?
- Kumbukumbu 7:6 & Wakolosai 3:11
- Je! Tunairithi nchi au mbingu?
- Mathayo 5:5 & Wakolosai 1:3-5
- Je! Kuja kwa Bwana utakuwa ni wakati wa hofu au faraja?
- Yoeli 2:1-11 & 1 Wathesalonike 4:16
- Je! Tunategemea utawala wa kidunia au wa kimbingu?
- Wafilipi 3:20 & Mathayo 6:10
- Je! Tutavumilia au tutaokolewa katika ghadhabu?
- Mathayo 24:13 & 1 Wathesalonike 1:10
- Je! Ni majembe au panga?
- Yoeli 3:10 & Mika 4:3
- Je! Baraka za kimwili au baraka za kiroho?
- Luka 12:32 & Waefeso 1:3
- Je! Upatanisho ni wa baadaye au ni wa sasa?
- Matendo 3:19 & Warumi 5:11
- Je! Neema ni ya baadaye au ni ya sasa?
- 1 Petro 1:13 & Warumi 5:2
- Je! Tutatawala mbinguni au duniani?
- Luka 22:30 & Waefeso 2:6
Ukinzani Juu ya Maombi
- Je! Ni mara ngapi tunatakiwa kuomba kabla ya kujibiwa?
- Isaya 65:24 & Waefeso 6:18
- Je! Tunapata vyote katika vile tuviombavyo?
- Mathayo 21:22 & 2 Wakorintho 12:8-9
- Je! Tunapaswa kufundishwa jinsi ya kuomba au la?
- Luka 11:1 & Warumi 8:26
- Je! Tunakipata kile tunachokiomba au zaidi ya hicho?
- Mathayo 21:22 & Waefeso 3:20
- Je! Mitume walikuwa na uwezo wa kuponya?
- Marko 16:18 & 1 Timotheo 5:23
- Je! Tunaweza kutarajia uponyaji kutoka kwa Mungu?
- Isaya 53:5 & 2 Wakorintho 12:7-10
Ukinzani wa Jumla
- Je! Uumbaji ulikuwa mzuri au mbaya?
- Mwanzo 1:31 & Mwanzo 6:6
- Je! Watakatifu wa Yerusalemu walikuwa maskini au matajiri?
- Matendo 4:34 & Warumi 15:26
- Je! Tunahitaji kufundishwa ‘Mjue Bwana’?
- Yeremia 31:34 & 1 Timotheo 4:10-11
- Tumeoshwa kwa maji au kwa Roho wa Mungu?
- Matendo 22:16 & 1 Wakorintho 6:11
- Je! Ni upendo mkubwa kufa kwa ajili ya rafiki zako au maadui?
- Yohana 15:13-14 & Warumi 5:10
- Je! Tunatufundishwa na malaika au tunawafundisha?
- Zekaria 1:9 & Waefeso 3:10
- Je! Yesu alikuwa jiwe likwazalo au jiwe kuu la pembeni?
- Warumi 9:33 & Waefeso 2:20
Angalizo:
Orodha hii si orodha kamilifu (exhaustive). Unaweza kuiendeleza kwa kadiri Roho wa Kristo atakavyokuongoza! Lakini pia, orodha hii haikusudiwi kuleta shaka juu ya ukweli wa Biblia. Ukitii AGIZO la kuigawa kweli ya Neno la Mungu sawasawa, kama ilivyoagizwa katika 2 Timotheo 2:15, hutatua kila aina ya mkanganyiko uliotajwa hapo juu.
Kwa Utukufu Wake Kristo Yesu
Leave a Reply