Home 2020 February 10 Huduma ya Yesu Katika Mwili

Huduma ya Yesu Katika Mwili

Huduma ya Yesu Katika Mwili

Huduma ya Yesu na Wanafunzi Kumi na Mbili

Bwana wetu Yesu Kristo alikuja kujionyesha Yeye kuwa ndiye Masihi-Mfalme kwa Taifa la Israeli. Maandiko yanatupa habari za kutosha juu jambo hili na matukio yatakayozunguka kuzaliwa kwake na huku ndiko kunakoleta maana ya Huduma yake. Na hili ndilo tangazo la kuzaliwa kwake Yesu, Malaika alilomletea Mariamu:

“Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanaume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha Daudi, baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:30-33).

Tangazo hili la Malaika lilikamilisha yale ambayo yalinenwa na manabii miaka mia nyingi iliyopita. Wayahudi kwa miaka mingi walitamani na kumsubiri mfalme mwenye haki kuja kuwaokoa kutoka kwenye mikono ya kutawaliwa na watu wa Mataifa na kuwarejeshea ufalme wao. Mfalme huyu na ufalme wake ungekuwa unatimiza unabii wa Musa na ahadi ya Mungu kwamba Taifa la Israeli litakuwa ni ‘kichwa na sio mkia’ (Kumbukumbu la Torati 28:13). Mariamu akajibu salamu hizi njema kwa shangilizo kuu:

“Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake in takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa hao wanaomcha. Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao; Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyone amewakweza. Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele” (Luka 1:46-55).

Kila Mariamu alilolisema katika shangilizo lake hilo, lilikuwa ni kumbukumbu ya ahadi za agano ambazo Mungu alikuwa amezifanya na Taifa la Israeli tangu wakati ule Mungu anamwita Ibrahimu. Mariamu hakusema lolote kumhusu yeye, bali Taifa lake. Zakaria naye, baba wa Yohana Mbatizaji, naye alifanya shangilizo kama hilo kufuatia kuzaliwa kwa mwanaye:

“Na wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakisema, Mtoto huyu atakuwa wa namna gani? Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye. Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema, Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa. Ametusimamishia pembe ya wokovu katika mlango wa Daudi, mtumishi wake. Kama alivyosema tangu mwanzo kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia; Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu; Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu, Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu, Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zote. Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu, Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake; Uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao. Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia. Kuwaangazia wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani” (Luka 1:66-79).

Msisitizo wa mashangilizo haya ni juu ya Agano la Mungu na ahadi za kinabii zilizotolewa kwa Israeli kama taifa. Kwamba mfalme na ufalme uliosubiriwa kwa muda mrefu sana, hatimaye sasa upo karibu Kuwasili. Uelewa huu pia, kwa ukamilifu wake, alikuwa nayo Nabii Yohana Mbatizaji na ndio ulikuwa ujumbe wake kwa taifa hilo. Mathayo anaandika hivi kumhusu Yohana:

“Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 3:1-2).

Na Bwana Yesu mwenyewe alitangaza ujumbe huo huo:

“Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu wale waliokaa katika giza wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia. Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, akisema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia“(Mathayo 4:12-17).

Jambo moja la kusitahajabisha kidogo katika mistari yote hiyo, wokovu kutoka kwenye dhambi zao kumesemwa kwa uchache sana. Kwa mwonekano huo inashangaza kidogo, lakini ukitafakari kwa undani, sivyo. Wakati kuna mamia ya misitari kwenye Agano la Kale ambayo inatangaza kusudio la Mungu kuanzisha ufalme wa Mungu katika taifa la Israeli, ni Sura moja tu ndiyo inayozungumzia jinsi Mungu atakavyo shughulika na dhambi zao, nayo haikueleka. Hii ni Isaya 53:

“Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:4-6).

na tena …,

“Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji” (Isaya 53:12)

Mwelekeo, mtizamo, mkazo wa Huduma ya Yesu ulikuwa ni kwa Wayahudi tu (Warumi 15:8). Aliwaamuru wanafunzi wake wasiende katika njia ya Mataifa, wala wasiingie katika mji wowote wa Wasamaria (Mathayo 10:5-7). Yeye mwenyewe binafsi hakuwa na mahusiano yoyote na jamii isiyo ya Kiyahudi, lakini katika maeneo michache sana ambayo yalikuwa hayakwepeki. Tunao mfano wa yule mwanamke Mkananayo (Mathayo 15:21-28; Marko 7:24-30) na yule akida aliyemjilia kwa ajili ya mtumishi wake (Mathew 8:5-13; Luke 7:1-10).

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *