SAULI WA TARSO – KIELELEZO CHA “NEEMA” YA MUNGU ILIYOZIDI SANA!
Katika barua yake kwa mwanawe wa kiroho, Timotheo, Mtume Paulo aliandika maneno yaliyonukuliwa hapa chini, takribani miaka 2000 iliyopita, kuhusu kuongoka kwake; Alisema:
“[Mimi] hapo awali nalikuwa mtukanaji na mtesaji na mwenye jeuri na mdhulumu; NA NEEMA YA BWANA WETU ILIZIDI SANA, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu…” (1 Timotheo 1:13-14)
Kufuatana na hili, linakuja lile tamko maarufu; Akisema:
“HILI NI NENO LA UAMINIFU, NA LINASTAHILI KUKUBALIKA KABISA, YA KWAMBA KRISTO YESU ALIKUJA ULIMWENGUNI ILI KUWAOKOA WENYE DHAMBI, AMBAO WA KWANZA WAO NI MIMI” (Mstari wa 15).
Baada ya kuyasoma maneno haya yaliyovuviwa ya Mtume Paulo, wale wanaozijua vyema Biblia zao, watakumbuka mara moja maneno ya Warumi 5:20-21; Kwamba:
“…sheria iliingia ili kosa liwe kubwa zaidi; LAKINI DHAMBI ILIPOZIDI, NEEMA ILI KUWA NYINGI ZAIDI; ILI KWAMBA, KAMA VILE DHAMBI ILIVYOTAWALA…, VINYO HIVYO NEEMA INAWEZA KUTAWALA…”
Vifungu hivi viwili kutoka kwenye kalamu ya Mtume Paulo, vina uhusiano wa karibu zaidi kuliko vinavyoweza kuonekana kwa juu juu. Mtume Paulo, wakati mmoja akiwa Sauli wa Tarso, alikuwa ameliongoza taifa lake na ulimwengu wote katika uasi dhidi ya Kristo. Kwa habari ya Sauli wa Tarso, tunasoma katika Matendo 8:3 kwamba, “aliharibu kanisa,” na yeye mwenyewe alishuhudia hayo kwa Wagalatia; Aliposema: “Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu” (Wagalatia 1:13).
Lakini Mungu, kwa rehema yake isiyo na kikomo, aliweza kumwokoa huyo Sauli wa Tarso; na sio kwa ajili ya Sauli kipekee, bali ili kumfanya awe KIELELE [ONYESHO] HAI CHA/LA NEEMA YAKE. Hivyo katika kumwandikia Timotheo, Mtume Paulo anaendelea kueleza:
“LAKINI KWA AJILI HII NALIPATA REHEMA, ILI KATIKA MIMI WA KWANZA, YESU KRISTO AUDHIHIRISHE UVUMILIVU WAKE WOTE; NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE, WAPATE UZIMA WA MILELE” (1 Timotheo 1:16).
Hima sote, na tuchukue nafasi zetu pamoja na Sauli wa Tarso, mwenye dhambi, na tupate wokovu kwa neema kupitia Kristo Yesu, Mwokozi wetu. Nami, nakuhimiza wewe kuwa; “Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka” (Matendo 16:31).
Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA
Leave a Reply