Home 2023 May 25 NGUVU INAYOTIMILISHWA KATIKA UDHAIFU

NGUVU INAYOTIMILISHWA KATIKA UDHAIFU

NGUVU INAYOTIMILISHWA KATIKA UDHAIFU

Kwa Paulo ulikabidhiwa ufunuo mkuu zaidi wa wakati wote. Aliagizwa kimungu kutangaza utoshelevu mtukufu wa kazi ya ukombozi ya Kristo, toleo la Mungu la wokovu kwa neema ya bure kwa wote wanaomtumaini Kristo na nafasi yao ya mbinguni, baraka na matarajio.

Ili asije akajivuna na utukufu wa kweli hizi kuu, Mungu alimpa kile anachokiita “mwiba katika mwili”, udhaifu wa kimwili wenye kuzidisha zaidi ‘maumivu’ ya aina fulani. “Kwa ajili ya jambo hili,” anasema, “nalimsihi Bwana mara tatu (3) kwamba kinitoke” (2 Wakorintho 12:8). Lakini Bwana alijua zaidi kuliko Mtume Paulo juu ya kile ambacho kilikuwa bora kwake:

“Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu” (Mstari wa 9)

Ni jinsi Mungu alikuwa sahihi! Kila Mkristo anajua kwamba penye “afya tele” na “bahati nzuri” huja tabia ya kusahau hitaji letu la kumtegemea Mungu, wakati udhaifu unatufanya tumtegemee Mungu zaidi na kuomba bila kukoma na hapa ndipo zilipo nguvu zetu za kiroho. Kila mwamini anapaswa kukiri hili na kusema pamoja na Paulo:

“Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu” (2 Wakorintho 12:9-10)

Udhaifu wa mwili ni wa kawaida hata kwa watakatifu wateule wa Mungu. Ni uradhi ulioje, basi, katika kuamini tu Neno la Mungu: “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hukamilishwa katika udhaifu“.

UTUKUFU NA UWEZA VINA YEYE MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *