Hadhi ya Mungu
Hadhi inahusu jinsi wengine wanavyokuona.
Mungu Mwenyezi ni mwenye hadhi kuu sana na yenye utukufu. Mungu ndiye aliyeviumba vitu vyote kwa uwezo wake yeye mwenyewe. Yeye ni wa milele, hana mwanzo wala mwisho. Yeye yu juu ya mataifa yote, na utukufu wake uko juu ya mbingu. Yeye ndiye mwenye haki, Mtakatifu, mwenye upendo na ni mwingi wa neema na rehema.
Mwanadamu ana hadhi ya chini. Mwanadamu ameumbwa kutoka kwenye udongo (mavumbini). Amezaliwa akiwa na udhaifu na ni mwenye shida nyingi. Wachache ndio wanakuwa wenye nguvu au wenye busara ya kutosha kutawala juu ya biashara moja, wachache zaidi ndio wanaokuwa na uwezo mkubwa kidogo wa kutawala juu ya taifa moja. Maisha ya mtu wa kawaida yapo katika ubatili, kiburi, dhambi, na majivuno.
Wakati ule Mungu alipojidhihirisha katika mwili, Yeye alijifanya mwenyewe kuwa hana hadhi. Ingawa Yeye hakuwahi kuacha kuwa Mungu, wala hakuwa Mungu mdogo. Hakuwahi kujiondolea, au kujivua, au kuweka pembeni moja ya hadhi zake kama Mungu.
Alijifanya mwenyewe kuwa hakuwa na hadhi yoyote:
“Ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu” (Wafilipi 2:6-7)
Kukosa Hadhi
Hadhi inahusu jinsi wengine wanavyokuona.
Wakati Mungu alipojidhihirisha na kuonekana katika mwili, kile walichokuwa wakikiona hakikuweza kuonekana kuwa ni kiumbe cha umilele ambacho ndicho kilikuwa kimeumba vitu vyote (vinavyoonekana na visivyoonekana) na kuishi nje ya muda na sayari.
Wakati watu wasioamini walipomwona Yesu, walimwona kuwa ni mtu mwenye hadhi kama mtu mwingine ye yote yule. Lakini wakati waumini walipomwona Yesu, walikuwa wakiuangalia ukamilifu wa Uungu katika mwili ambao ulijiona hauna hadhi.
Kwa nini Mungu alijifanya yeye mwenyewe kuwa hana hadhi yoyote ile katika mfano wa mwanadamu? Kwa nini mtu yeyote yule angetaka kupunguza hadhi yake kiasi hicho, achilia mbali kuwaruhusu watu wengine wamtemee mate juu yake (Luka 18:32)?
Ukamilifu wa Uungu katika mwili, katika mtindo wa kama mtu mwenye hadhi ya chini, kutuhumiwa kwa makosa ya uwongo dhidi yake mwenyewe, alikufa akiwa mnyenyekevu juu ya msalaba, akiwa uchi na tena karibu na wezi. Mungu hakuwa tu hana hadhi, lakini alionekana pia kukosa heshima (kuheshimiwa).
Hadhi inahusu jinsi wengine wanavyokuona. Kumwangalia Yesu msalabani, hadhi yake ya chini kama mwanadamu haikustahili asili yake kama Mungu. Alikuwa na hadhi ya kufa kama mdhambi, ingawa Yeye hakuwahi hakujua dhambi.
Hadhi ya Mungu Yarejea
Hadhi yake isingeendelea kubaki chini hivyo.
Yesu, akiwa Mungu, alifufuka kutoka kwa wafu na kupaa mbinguni katika mwili wa utukufu. Hadhi ya Mungu ilianza kubadilika na kuimarika kwa kadiri ilivyokuwa ikuhubiriwa na Mitume kwamba Mungu aliyejidhihirisha katika mwili alikuwa ni vyote; Bwana na Kristo (Matendo 2:36).
Hadhi ya Mungu iliimarika zaidi pale alipojitokeza akiwa katika utukufu wake ili kumwokoa mdhambi mmoja asiyestahili wokovu (Matendo 9:4).
Hadhi inahusu jinsi wengine wanavyokuona, na Paulo alimwona Bwana aliyefufuka katika utukufu wake, ulio mkuu kuliko vitu vyote, kulingana na ufunuo wa ili siri (Waefeso 1:9-10; Warumi 16:25). Paulo alitumwa kuhubiri HADHI YA MUNGU iliyoinuliwa JUU SANA katika Kristo.
Mungu aliyejidhihirisha katika mwili, hakuwa tu Muumba, Bwana, na Kristo, lakini sasa alikuwa akijulikana kama Mwokozi wa watu wote, Mkuu wa Kanisa, aliyeinuliwa juu ya vitu vyote, mbinguni na duniani (Wafilipi 2:9-11)!
“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”
Mungu ambaye hapo awali alikuwa na hadhi ya juu sana, na baadae akajifanya yeye mwenyewe kuwa hana hadhi, sasa ana hadhi kubwa zaidi kuliko hapo awali. Yeye amekuwa ndiye mwenye haki na mwenye kutoa haki pekee, hakimu na mpatanishi, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo (Tito 2:13).
Hadhi Kuu (ya Juu zaidi) ya Mungu
Kitu cha kujisifia juu ya hadhi ya Mungu, iliyo kubwa sana, ni kwamba sasa tunajua ni kwa nini Mungu alijifanya kuwa hana hadhi yoyote. Sasa ni dhahiri kwamba Mungu alijifanya hakuwa na hadhi yoyote ile kwa ajili ya wenye dhambi!
Alikuwa yuko tayari kuonekana kuwa hana hadhi yoyote ile, ili aweze kuwaokoa wale waliokuwa hawana hadhi (walikuwa na hadhi ya chini). Ndio kusema, Kristo aliuthamini wokovu wetu kuliko hadhi yake!
Mungu hakuwa ameachilia, au amejivua, au ameondoa, au kuweka pembeni chochote katika hadhi yake ya Mungu wakati ule yeye alijidhihirisha katika mwili. Alijua kile alikuwa akifanya yote pamoja na hadhi ya utukufu wake.
Mungu alijivisha mfano wa ubinadamu, wenye dhambi, ili aweze kutoa wokovu kwa hao wenye dhambi, kama Mwokozi aliyefufuka.
Kwa Utukufu wa Kristo
Leave a Reply