Home 2020 July 22 Agizo la Paulo kwa Timotheo

Agizo la Paulo kwa Timotheo

Agizo la Paulo kwa Timotheo

Kwanini Paulo Alimwagiza Timotheo “Kuigawa Kweli ya Neno la Mungu” Sawasawa?

Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Timotheo 2:15)

Pengine umewahi kuusikia mstari huu ukitumika kama motto (slogan) kwa ajili ya mafunzo ya Biblia au katika kuisoma Biblia kulingana na wakati/majira au hadhira, lakini swali linabaki kuwa: Ni kwanini Paulo alimwagiza Timotheo kulitumia kwa halali neno la kweli (kuigawa kweli ya neno la Mungu sawasawa)?

Paulo alimaanisha nini kwa kusema “litumie kwa halali neno la kweli”?

Katika mstari uliotangulia kabla ya agizo hilo (pre-text), tunaona kwamba kulikuwa na ‘mabishano’ juu ya neno la Mungu ambayo yaliwapotoa wasikilizaji wake na kuharibu imani yao:

“Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao” (2 Timotheo 2:14)

Agizo la Paulo kwa Timotheo kulitumia kwa halali neno la kweli lililenga kuwaokoa watu hawa (wasikiaji wa mabishano yale) kutoka kwenye ‘upotovu’ kwa kuwakumbusha mambo hayo!

Swali linalokuja hapo, ni kwamba: Kuwakumbusha mambo hayo; yepi?

“Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote. Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili yangu” (2 Timotheo 2:7-8)

Walitakiwa wakumbuke kuwa Paulo alichaguliwa kuwa Mhubiri, Mtume na Mwalimu wa Mataifa, na walitakuwa kudumu katika yale waliyojifunza kutoka kwake:

“ambayo kwa ajili ya hiyo naliwekwa niwe mhubiri na mtume na mwalimu. Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile. Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu” (2 Timotheo 1:11-13)

Injili ya Paulo pekee ndiyo itoayo ufafanuzi kamili wa nini lilikuwa kusudi la KIFO cha Yesu na KUFUFUKA kwake, ambalo lilikuwa limefichwa kwa Mungu tangu kuwako kwa misingi ya dunia, lakini sasa limefuniliwa kwa Paulo kulihubiri:

“Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili; ambayo kwa ajili ya hiyo naliwekwa niwe mhubiri na mtume na mwalimu” (2 timotheo 1:8-11)

Paulo alivumilia mateso mengi katika kuihubiri SIRI ya Injili ya Kristo aliyowekewa yeye amana hiyo na Bwana baada ya ufufuko wake:

“Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili! Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili” (1 Wakorintho 9:16-17)

 “pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili; ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena” (Waefeso 6:19-20)

Kwa neema ya Mungu, Paulo alihimili mateso hayo ili aweze kuona watu wote wafaidike kwa uzima wa milele na utajiri (ukubwa) wa neema ya Mungu sawasawa (unaopatikana kutokana) na ‘injili yake’. Ilikuwa ni kutokana na injili ya Paulo’ pekee, ambamo sasa watu wangeweza kupata faida hiyo inayopatikana katika Kristo.

Timotheo alikuwa na wito huo huo kutoka kwa Paulo (1 Timotheo 6:20-21), lakini badala ya kuwafaidisha wasilikizaji wake; walikuwa wakipotoshwa!

Kulikuwa na baadhi ya watu waliotamani kuwa walimu wa sheria ambayo Paulo aliita ni ubatili na wengine walifundisha unajisi/uharibifu/uchafuzi (profanity) kwa kuukataa ufufuko wa Kristo:

“Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki. Wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili; wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti. Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali; akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji” (1 Timotheo 1:5-9)

Neno la kweli, lililotumiwa kwa halali, lilitakiwa liwalete watu wote kwenye uelewa wa kusudi la Mungu. Kinyume chake kimetokea, kwa sababu ya fundisho baya (mafundisho yasiyo na uzima).

Timotheo alikabiliwa na shinikizo la kubadilisha fundisho la imani alilojifunza kutoka kwa Paulo, na pengine kuyafuata mafundisho ya Musa, Yesu chini ya sheria, au ya kutahiriwa.

Paulo alimhimiza/alimwonya Timotheo kutokumwonea aibu Bwana wetu, yeye Paulo, wala ujumbe wa neema ya Mungu aliojifunza kwake, bali awe/asimame imara/hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu (2 Timotheo 1:8; 1:13; 2:1).

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *