Home 2020 February 03 Je ninini maana ya kuzaliwa Mara ya Pili

Je ninini maana ya kuzaliwa Mara ya Pili

Je ninini maana ya kuzaliwa Mara ya Pili

Je kwa mkristo ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili? Sehemu muhimu katika Bibilia inayo jibu swali hili ni Yohana 3:1-21. Bwana Yesu Kristo akizungumza na Nikodemo mkuu kati ya mafarisayo na mfuasi katika kikao (mahakama) kikuu cha wayahudi (Mfalme wa wayahudi). Nikodemo alikuwa amemjia Yesu usiku. Nikodemo alikuwa na maswali ya kumuuliza Yesu. Wakati Yesu akizungumza na Nikodemo, alisema, “Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.  (Yohana 3:3-7). Msemo kuzaliwa mara ya pili unamaanisha zaliwa toka juu, Nikodemo alikuwa na uhitaji wa kweli. Alihitaji mabadiliko ya moyo wake. Mabadiliko ya kiroho ni uzao mpya, kuzaliwa mara ya pili, ni kitendo au hatua ya Kiungu ambapo mtu hupewa uzima wa milele yule aaminiye (2Wakorintho 5:17; Tito 3:5; 1Petro 1:3; 1Yohana 2:29; 3:9; 4:7; 5:1-4, 18).

Yohana1:12, 13 inasema ya kuwa kuzaliwa mara ya pili ina maana kufanyika mtoto wa Mungu kwa imani katika jina la Yesu Kristo. Swali hasa ni kuwa, kwa nini mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili? Mtume Paulo katika Waefeso 2:1 asema, “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi”. Kwa Warumi katika Warumi3:23, Mtume Paulo aliandika, “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”. Kwahivyo mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili ili asamehewe dhambi zake na awe na uhusiano na Mungu. Je, hii hutokea vipi? Waefeso 2:8-9 yasema, “kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu”.

Mtu anapo okolewa, basi yeye amezaliwa mara ya pili, akijazwa upya kiroho, na sasa amefanyika kuwa mwana wa Mungu kwa haki ya uzao mpya. Kwa kumwamini Kristo Yesu, yeye aliye adhibiwa kwa ajili ya dhambi alipokufa msalabani, ndiyo maana ya kuzaliwa mara ya pili kiroho. Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya (2Wakorintho 5:17a). Kama bado hujaweza kumwamini Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, je utakuwa na utayari wa kumpokea Roho mtakatifu wakati akizungumza na moyo wako? Unahitaji kuzaliwa mara ya pili. Je, unaweza kuchukua hatua ya Imani na kufanya maombi ya kutubu na ufanyike kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo hivi leo? “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13).

Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako na uzaliwe mara ya pili, fuatiza mfano huu wa maombi kwa imani. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumweleza Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kupewa wokovu, tena bure. “Mungu wangu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa uovu wangu. Ninaziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha wa dhambi zangu, Amina”!

Author: magebo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *