Sisi Tunaamini…
– Mungu Mmoja, Nafsi Tatu:
Mungu ni Mmoja, yupo katika nafsi tatu. Nafsi hizo tatu zipo katika umoja, kila nafsi moja ikiwa na sifa za Mungu.
– Uungu wa Yesu Kristo aliyezaliwa na Bikira akiwa mtu kamilifu, na Mungu kamilifu aliyejidhihirisha katika mwili.
– Upatanisho wa mbadala wa Kristo kwa ajili ya wokovu wetu, kwa neema pekee, kwa njia ya imani pekee, katika Kristo pekee.
– Ufufuo halisi wa Kristo ili kutoa wokovu na uzima wa milele kwa wote wanaoamini.
– Kurudi kwa Kristo kimwili ili kutawala mbinguni na duniani
Kinachotufanya tuwe wa kipekee miongoni mwa Wakristo:
Sisi Tunaamini…
Tunaamini uwakili wa Paulo kwa Kanisa Mwili wa Kristo
Yesu Kristo alimpa Mtume Paulo injili mpya, na tofauti – ufunuo wa ile siri – ambayo ina maelekezo kamili kwa Kanisa katika majira haya.
Katika kipindi hiki cha neema ya Mungu, sisi hatupo chini ya sheria
Uhusiano wa kifamilia ni mtazamo wa Mungu na Kanisa
Sisi sote tuna jukumu la kufanya maamuzi yetu mbele ya Mungu. Hakuna ukuhani leo. Kristo ndiye mpatanishi pekee.
Nguvu za Mungu hufanya kazi kupitia mafundisho yenye uzima ili kuleta mabadiliko chanya katika ulimwengu
Mabalozi wa Mungu huishi katika ulimwengu lakini hawapaswi kuishi kama ulimwengu
Wokovu:
Sisi Tunaamini…
Tunaokolewa kutoka kwenye dhambi na kifo tunapoamini katika kazi iliyo kamilika ya Yesu Kristo juu ya msalaba na ufufuo wake wa kimwili. Damu yake isiyo na dhambi hulipa deni la dhambi zetu, hutupa msamaha, na kutupatia uzima wa milele.
Kwa hiyo, wokovu sio zao la:
– Maombi
– Ubatizo
– Kutubu Dhambi
– Kazi Njema
– Kuacha Dhambi
– Sheria/Maagizo
– Uwanachama katika Kanisa
– Ibada au Meza ya Bwana
Bali, Wokovu hupatikana bure, kwa waovu wote ambao wataweka imani yao katika kifo, damu, kuzikwa, na kufufuka wa Yesu Kristo kwa ajili ya dhambi zao (Warumi 4:5; Warumi 4:24-25; 1 Wakorinto 15:1-4).