Home 2020 March 29 Kanisa Bila Paulo

Kanisa Bila Paulo

Kanisa Bila Paulo

Kuna msemo maarufu unaosema, “hujui thamani ya kitu ulichonacho, mpaka pale kitu hicho kinapokuondoka.” Kwa muda mrefu sana ufunuo maalum wa Bwana kwa Paulo umepata mwitikio wa pili, kama sio wa tatu, dhidi ya “maandishi mekundu ‘ na unabii.

Hebu tujifanye kuwa Paulo kamwe hakuokolewa katika barabara ya Dameski. Je, umewahi kujiuliza kuwa ni nini kingetokea kwa Kanisa kama Paulo hakuwahi kupewa ufunuo wake wa siri kutoka kwa Bwana?

Ondoa kwa muda nyaraka za Paulo kutoka kwenye Biblia. Kuna vitabu kumi na tatu kutoka Warumi hadi Filemoni, viondoe vyote. Pia utahitaji kuondoa sehemu inayohusu huduma ya Paulo katika Kitabu cha Matendo ya Mitume; yaani kuanzia Matendo ya Mitume Sura ya Tisa na kuendelea, inapaswa pia kuondolewa.

Sasa, hebu na tuchore picha halisi ya kile kinachobakia…!

KANISA BILA PAULO

Bila Paulo, ushuhuda wa mwisho kutoka kwa Kanisa tunaouona ni wa Kanisa likiwa Hekaluni, kuanzia Sura ya 2-5 ya kitabu cha Matendo ya Mitume. Kundi hili linaongozwa na Mtume Petro na wale Mitume wengine kumi na moja.

Wao walikuwa wakiendelea kutekeleza agizo la Bwana katika Marko 16, Mathayo 28, Luka 24, and Yohana 20. Kilichoandamana na huduma yao ilikuwa ni nguvu za ajabu (dalili nyingi) ambazo Roho Mtakatifu alikuwa akizitumia kama ishara za ufalme unaokuja (Marko 16:17).

Yesu alikuwa amewaagiza Mitume (wanafunzi wake) katika mwisho wa huduma yake kubaki katika Yerusalemu mpaka hapo watakapo pokea nguvu kutoka juu, kisha waende Yudea, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Kufikia Matendo 8 Kanisa lilikuwa limetawanyika isipokuwa kwa wale Mitume ambao walikuwa ‘watiifu’ kwa maelekezo waliyopewa (Matendo 8:1).

Katika kufuata nyayo za Petro, ujumbe tunaoufundisha ni kuwa ‘hizi ni siku za mwisho’, ‘tubuni na mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu’, na kuhubiriwa kwa msalaba itakuwa ni kuonyesha kana kwamba yalikuwa ni mauaji ya kutisha ya Masihi (Matendo 2:17, 38, na Matendo 5:30).

Tutahitaji pia kufuata maelekezo ya Bwana, na kufuata pia mfano wa Mitume (Wanafunzi wa Yesu), kwa kuuza vyote tuliyo navyo na kuwa na vitu vyote shirika (Luka 12:33, Matendo 2:45; 4:34).

Wokovu ungekuwa ni wa Wayahudi tu (Yohana 4:22), nasi tungekuwa tunashiriki katika kuuleta ufalme ambao utakuwa unasubiri kurudi kwa Bwana kwa Israeli (Matendo. 1:6, Isaya 2:2-4).

Usingeweza pia kuuelewa msalaba (Luka 18:34), na ungetakiwa kuwa na imani kwa Yesu ambaye ni Masihi na matendo ya sheria kwa ajili ya kuhesabiwa haki (Yakobo 2:24).

Kitu ambacho kamwe usingeweza kukifanya, ingekuwa ni kwenda kwenye nyumba ya Myunani ambaye hakuwa mtauwa, hakuwa mchaji wa Mungu (Matendo 10).

Bila shaka, kwa sababu imekuwa karibu miaka 2000 tangu Petro alipotamka kwa mara ya kwanza madai ya ‘siku za mwisho’, sasa inaweza kuwa ni wakati mzuri zaidi wa kutathmini upya mpango mzima wa kinabii wa ufalme wa Kiyahudi. Ahadi za Mungu, pengine zimekuwa ni za bure (Warumi 9:6)?

MAANDIKO YA PAULO PEKEE

Si ajabu kuona huduma ‘bila Paulo’ inavyolielezea Kanisa la kisasa (la leo) ambalo halijatoa nafasi ya ofisi ya Paulo kama mtume wao (Warumi 11:13).

Bila maandiko ya Paulo hutaweza KUTHIBITISHA mafundisho ya msingi, kama vile:

– Wokovu kwa neema kupitia imani

– Kuhesabiwa haki bila sheria

– Upatanisho kamili kupitia kifo na ufufuo

– Kanisa ni Mwili wa Kristo, ambamo Myahudi na Wayunani wako sawa

– Kuanguka kwa Israeli na ukimya wa kinabii wa Mungu kwa karibu miaka 2000

– Nafasi yetu ya kimbingu katika Kristo

Kama vile Mwanathiolojia mmoja alivyowahi kusema takribani karne moja iliyopita, “katika maandiko ya Paulo peke yake tunapata fundisho, nafasi, mwenendo, na hatima ya Kanisa.” Kuondoa maandiko ya Paulo kunafanya ukweli huu, kuwa ukweli ulio wazi!

Ni kwa kiwango kidogo sana tunathamini ujumbe ambao Yesu alimpa Paulo autoe/auweke kwetu (kwa Kanisa), na muundo wa huduma tulionao kupitia maandiko ya Mtume Paulo (1 Wakorinto 9:17, 1 Timotheo 1:16). Muda umewadia sasa kwa Kanisa kutii maelekezo ya Yesu ya “kumfuata Paulo” (1 Wakorinto 4:16).

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *