Home 2020 March 15 Waambie Wengine Kuhusu Injili

Waambie Wengine Kuhusu Injili

Waambie Wengine Kuhusu Injili

Kama umeokolewa unaijua injili ya Kristo!

Hili ni jambo la msingi, na lipo katika kila shina la ujumbe wa nyaraka za Paulo.

Kristo alifanya kila kitu muhimu kilichohitajika ili kukuokoa kutokana na dhambi na kifo kupitia damu yake aliyoimwaga juu ya msalaba. Hakuna kitu kingine ambacho kinahitaji kufanywa kwa ajili ya wokovu wako. Hakuna agano, hakuna sheria, hakuna matendo, hakuna ubatizo, hakuna maombi, hakuna kingine kinachohitajika kukamilisha wokovu wako zaidi ya kile Yesu alichokifanaya. Wewe amini tu ‘msaada huu wa Mungu’ kwa ajili ya ukosefu wako.

Hii ni mada ya mazungumzo na marafiki zako ambao hawaelewi Biblia iliyogawanywa sawasawa. Huenda ikawa wamelelewa makanisani maisha yao yote lakini wakakosa kuijua injili hii rahisi.

Zungumza nao kuhusu hilo. Waambie jinsi ulivyo uzuri wa ajabu kwa vile hakuna kitu kingine kilichobakia kwa ajili ya kupata/kupokea wokovu wao. “Wakristo wasiookoka” ni uwanja mkubwa/mpana zaidi wa kufanya uinjilisti wa namna hii katika nchi yetu.

Watu pekee ambao wanaudhika/kukwazika na injili ni watu wasiookoka (2 Wakorinto 2:16, 4:3). Ikiwa umeweza kuwatambua kama ni ‘wajinga’ wa injili basi tambua kwamba ni újinga’ zaidi kuzungumza nao juu ya mambo ya ndani ya kiroho kama vile SIRI YA KRISTO.

Anza na injili. Utukufu katika injili. Simama katika hilo mpaka ujue wana uzima wa milele.

Kisha zungumza nao kuhusu kuamini Biblia yao!

Kwa utukufu wake Kristo Yesu

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *